DAR-Bao la kichwa la dakika ya mwisho lililofungwa na Kibu Denis limeiwezesha Simba Sports Club kupata pointi tatu muhimu nyumbani dhidi ya CS Sfaxien.
Ni baada ya ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo Kombe la Shirikisho barani Afrika uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Kibu alifunga bao hilo dakika ya mwisho ya nyongeza baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na kiungo mkabaji, Yusuph Kagoma.
Mshambuliaji Hazem Haj Hansen aliipatia CS Sfaxien bao la kwanza dakika ya tatu baada ya mlinzi Che Fondoh Malone kurudisha pasi fupi kwa mlinda mlango.
Aidha,Kibu aliwapatia Simba Sports Club bao la kusawazisha kwa kichwa dakika ya nane baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Jean Charles Ahoua.
Kipindi cha pili waliongeza kasi huku Sfaxien wakitumia muda mwingi kujiangusha na kupoteza muda.
Mabadiliko aliyofanya kocha Fadlu Davids kipindi cha pili ya kuwaingiza Valentine Nouma, Kagoma, Joshua Mutale na Steven Mukwala yaliongeza kasi na kutufanya kuongeza mashambulizi mengi langoni mwa Sfaxien.
Wakati huo huo, katika kikosi kilichoikabili CS Sfaxien katika mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, Kocha Fadlu Davids amefanya mabadiliko ya wachezaji wawili ukilinganisha na kikosi kilichocheza mechi iliyopita dhidi ya CS Constantine.
Kocha Fadlu aliwaanzisha Debora Fernandes na Awesu Awesu kuchukua nafasi za Karaboue Chamou na Augustine Okajepha ambao leo wapo benchi.
Hiki hapa kikosi kamili:
Moussa Camara (40), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Che Malone (20), Abdulrazack Hamza (14), Fabrice Ngoma (6), Kibu Denis (38), Deborah Fernandez (17), Leonel Ateba (13), Jean Charles Ahoua (10), Awesu Awesu (23).
Wachezaji wa Akiba:
Aishi Manula (28), Valentine Nouma (29), Karaboue Chamou (2), Yusuph Kagoma (21), Mzamiru Yassin (19), Augustine Okajepha (25), Steven Mukwala (11), Ladaki Chasambi (36), Joshua Mutale (26).