DAR-Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imemkamata Bw. Kija Mayunga mkazi wa Dodoma anayedaiwa kuwatapeli ndugu wa wagonjwa kwa madai ya kuwasaidia ili wapate huduma.
Bw. Mayunga tayari amefikishwa Kituo cha Polisi Gogoni kwa hatua zaidi.
Kufuatia hali hiyo Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila unatoa wito kwa wananchi kufuata utaratibu wa kupata huduma ikiwemo kufuata utaratibu wa malipo uliowekwa na hospitali ili kuepuka matapeli.