ZANZIBAR-Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), Hemed Suleiman (Morocco) amewaondoa kwenye timu hiyo wachezaji Ibrahim Mkoko wa Namungo FC na Abdallah Said wa KMC FC kwa makosa ya utovu wa nidhamu.
Sambamba na kutofika kambini kwa wakati huku wakiwa wamesharuhusiwa na timu zao muda mrefu. Kocha huyo amemuongeza kwenye timu Ali Juma Maarifa (Mabata) kutoka Uhamiaji FC ya Zanzibar.