Kongamano la 11 la Kitaaluma la Chuo cha Ustawi wa Jamii lafana

DAR-Wadau, wanataaluma na wanafunzi wameshiriki kongamano la 11 la kitaaluma (convocation) juu ya uwezeshaji na ubunifu katika kubadilisha elimu kuwa fursa.
Akizungumza leo Desemba 5,2024 jijini Dar es Salaam, Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma - Prof. Sotco Komba amesema kongamano hili limekuwa ni fursa kwa wanafunzi kujifunza masuala ya ubunifu, ambapo katika maisha ya sasa ubunifu umekuwa kichocheo cha kuleta maendeleo katika jamii. Na kupitia Mada kuu iliyowasilishwa imeweza kufanya wanafunzi kuelewa dhana nzima ya ubunifu.
Dkt.Harun Makandi, Mratibu Tafiti Mwandamizi kutoka Idara ya Maendeleo ya Teknolojia Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania COSTECH amesema kuwa, wanafunzi waendelee kuwa wabunifu na wasibaki nyuma wajitahidi kuwashirikisha wadau mbalimbali na Taasisi zinazojihusisha na ubunifu ili waweze kukutanishwa na wawekezaji na kupewa miongozo ya kulinda bunifu zao.

Umekuwa ni utamaduni wa Chuo cha Ustawi wa Jamii kufanya kongamano hili la kitaaluma kila mwaka kabla ya mahafali , ambapo kwa mwaka 2024 maha

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

  1. Waende nyumbani wakatumie mahalifa yao vizuri

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news