ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewatakia Krismasi njema yenye upendo na mshikamano kwa familia na jamii kwa ujumla.
Aidha, amewasihi wananchi waendelee kuuenzi utamaduni wa kusherehekea msimu huu wa sikukuu kwa amani na utulivu, ambayo ni alama ya taifa letu.
"Krismasi njema na mapumziko mema yenye baraka tele."