Lengo letu ni kuhamia kwenye jengo jipya la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali mwezi Mei-Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali

DODOMA-Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Samwel Maneno amekutana na kufanya kikao na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), ambaye ni Meneja wa mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na SUMA JKT ambaye ni Mkandarasi anayesimamia mradi wa ujenzi wa jengo hilo, kwa lengo la kupata taarifa ya maendeleo ya mradi huo.
Kikao hicho kimefanyika, tarehe 20 Desemba, 2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mtumba Jijini, Dodoma.
Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ameweka bayana matamanio na matarajio ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa ni kuhamia katika jengo hilo jipya mapema Mwezi Mei 2025.

“Shabaha yetu ni kuhamia kwenye jengo hili jipya mwezi wa tano 2025, tunataka Watumishi wetu wahamie na kuanza kulitumia,”amesema Naibu Mwanasheri Mkuu wa Serikali.
Aidha, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali amemtaka Mkandarasi wa Mradi huo kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati ili jengo hilo lianze kutumika, huku akimuhakikishia kuendelea kumpatia ushirikiano na kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya mradi huo.

“Napenda kuwahakikishia kuwa tutawapa ushirikiano wa kutosha ili mtekeleze majukumu yenu kwa urahisi na tutaendelea kufuatilia kwa ukaribu sana maendeleo ya ujenzi wa jengo hili,”amesema Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Awali akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Meneja wa mradi huo kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Bw. Ng’olo Waje amesema kuwa mpaka sasa mradi huo umefikia asilimia 70, huku akiahidi kuendelea kuusimamia mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati.

“Kwa upande wetu tunaahidi kuendelea kuusimamia mradi huu na kuhakikisha mkandarasi anaukamilisha kwa wakati," amesema Bw. Waje.
Kwa upande wake Mhandisi wa mradi huo kutoka SUMA JKT Eng. Evance A. Mwingizi amesema kuwa wanaendelea na hatua ya Umaliziaji wa jengo hilo, huku wakiwa tayari wameshaweka tiles ghorofa ya kwanza hadi ya tano, wameshafunga lift, wanaendelea na uwekaji wa vioo pamoja na partition”.

“Tunaendelea na kazi ya umaliziaji kwasasa hivi tunaweka vioo na kutengeneza partition za ofisi,"amesema Eng. Mwingizi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news