DAR-Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa taarifa kwa Watanzania kuhusu kuwasili kwa mabehewa ya mizigo 264 yaliyotengenezwa nchini China.
Mabehewa hayo yamewasili Desemba 24,2024 katika Bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya Reli ya Kisasa (SGR).
Kati ya mabehewa hayo, 200 yameundwa kwa ajili ya kubeba makontena, huku 64 yakibeba mizigo isiyofungwa (shehena kichele). Baada ya kushushwa kutoka kwenye meli, yatafanyiwa majaribio kwa kasi ya kilomita 120 kwa saa, yakiwa tupu na yakiwa yamebeba mizigo.