ZANZIBAR-Umoja wa Ulaya (EU) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wamesaini makubaliano mawili muhimu yanayolenga kukuza maendeleo endelevu, uhifadhi wa bahari na usawa wa kijinsia.
Makubaliano hayo yalisainiwa mbele ya Riziki Pembe Juma, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto; Rita Laranjinha, Mkurugenzi Mtendaji wa Masuala ya Afrika wa Huduma za Nje za Umoja wa Ulaya; na Hans Stausboll, Kaimu Mkurugenzi wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Kanda ya Afrika, pamoja na maafisa waandamizi wa serikali na wadau wa maendeleo.
Makubaliano ya kwanza, yenye thamani ya Sh bilioni 32, yanahusu uhifadhi wa bahari kupitia Mradi wa Bahari Yetu. Mradi huu, unaotekelezwa na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira (IUCN), unalenga kushughulikia changamoto muhimu za kulinda rasilimali za bahari, kukuza uvuvi endelevu, na kupambana na uchafuzi wa plastiki.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo