ZANZIBAR-Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi ametunukiwa tuzo ya Heshima katika usiku wa tuzo za Malkia wa nguvu zinazotolewa na Clouds Media Group.
Kwa upande wa Zanzibar wanawake wengine nane akiwemo mtoto wa Rais Samia Suluhu Hassan, Wanu Hafidh Amir waliibuka washindi katika tuzo hizo za kila mwaka.
Mama Mariam ni mwanzilishi wa taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) na Wanu ni mwanzilishi wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation.
Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Mhandisi Zena Said amewataka wanaume kwenye maeneo mbalimbali kuwapa ushirikiano wanawake hasa wenye maono makubwa ya kiuchumi na kijamii.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo