TABORA-Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi minane, Martin Ndalu, amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa baada ya kupigwa shoti baada ya kushika waya uliokuwa ukishikilia nguzo ya umeme katika Mtaa wa CG, Kata ya Kitete, Manispaa ya Tabora.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Richard Abwao, alisema tukio hilo lilitokea Jumanne saa 2:00 asubuhi.
Alisema, mtoto huyo alimtoroka dada yake na kwenda nje na kushika waya uliokuwa umeshikilia nguzo ya umeme na ndipo alipopigwa shoti.
Kamanda huyo alisema, wakati dada yake akimvuta ili kumwokoa alipigwa shoti akaanguka na walikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa Kitete, lakini mtoto Martin alifariki dunia na dada yake anaendelea kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo