DODOMA-Jeshi la Polisi limesema kuwa, linaendelea na ufuatiliaji wa tukio la kupotea kwa Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, Abdul Nondo.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Desemba 1,2024 na Msemaji wa jeshi hilo, David Misime ikieleza kuwa,saa 11 alfajiri ya jan katika eneo la Mbezi Luis, stendi ya mabasi ya Magufuli mwanaume mmoja alikamatwa kwa nguvu na watu waliotumia gari lenye namba za usajili T 249 CMV Land Cruiser nyeupe.
“Ilielezwa na mashuhuda kuwa katika purukushani za ukamataji begi dogo lilidondoshwa na baadhi ya vitu vilivyokuwemo vimetambuliwa vya Abdul Omary Nondo,” imeeleza taarifa hiyo.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo