ARUSHA-Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dk Pindi Hazara Chana amemuapisha na kumvisha cheo cha kijeshi Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, CC Dkt.Elirehema Joshua Doriye huku akimtaka kuitumia nafasi hiyo kuonesha utendaji uliotukuka na wenye tija kwa maslahi ya Watanzania wote.
Hayo yamejiri katika hafla ya kuvishwa cheo na kuapishwa kwa Kamishna Doriye iliyofanyika Makao Makuu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro tarehe 23 Desemba, 2024.
“Ni matumaini yetu makubwa kuwa utaendelea kutumia vipawa vyako kuhakikisha mafanikio makubwa yanapatikana katika mamlaka hii, hususani katika kipindi hiki ambacho sekta ya utalii inaendelea kushamiri duniani. Katika kipindi kifupi cha utendaji wako, tumeona mafanikio makubwa yanayodhihirisha uwezo wako,” amesisitiza Chana.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo