MAPUTO-Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Msumbiji, Bernadino Rafael amesema wafungwa 6,000 wakiwemo 29 ambao walihukumiwa kwa ugadi, walitoroka katika Gereza Kuu la Maputo siku ya Krismasi wakati wa maandamano kufuatia ushindi wa chama tawala cha Frelimo.
Rafael amesema,wafungwa 33 walikufa na wengine 15 walijeruhiwa wakati wa makabiliano na vikosi vya usalama.
Maandamano hayo, yaliyofanywa na wafuasi wa mgombea aliyeshindwa Venancio Mondlane, yalisababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya polisi na kuanguka kwa ukuta wa gereza.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Msumbiji Pascoal Ronda ameyahusisha machafuko hayo na mzozo wa matokeo ya uchaguzi, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akitoa wito wa mazungumzo na kukomesha vurugu.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo