Magazeti leo Desemba 29,2024

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili Mloganzila imemkamata Steven K. Julius kwa tuhuma za wizi wa mali za wa wagonjwa ikiwemo simu za wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo kwa kujifanya ni mwajiriwa wa Muhimbili Mloganzila kwa cheo cha Afisa Muuguzi.
Baada ya mahojiano Julius amekiri kuiba simu tatu ambapo mbili aliziuza kwa mkazi wa Kibamba na moja ameiuza kwa mtu anyeishi nje ya mkoa wa Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Bw. Julius baada ya kumaliza mafunzo kwa vitendo ya uuguzi (nursing internship) amefanya kazi katika hospitali kadhaa za mkoa wa Dar es Salaam ambapo alifukuzwa kutokana na vitendo vya kukiuka maadili ikiwemo wizi.
Mtuhumiwa amefikishwa Kituo cha Polisi Gogoni kilichopo Kibamba kwa taratibu za kisheria.

Aidha uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili inapenda kuihakikishia jamii kuwa inayo mifumo imara ya kiusalama ya kuweza kubaini watu wote wanaoingia na kutoka hospitalini na ndio maana imeweza kumfuatilia mtuhumiwa huyu na kumkamata.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news