Magazeti leo Desemba 3,2024

DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan ameongoza shughuli ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika,Dkt. Faustine Ndugulile katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Akitoa salamu za pole, Rais Dkt.Samia amesema,Dkt.Ndulile ameweka heshima kwa Tanzania kutokana na nafasi aliyoipata katika Shirika la Afya Duniani (WHO).
Amesema, kuondoka kwake ni kugumu lakini hiyo ni mipango ya Mwenyezi Mungu na kutaka Watanzania kulipokea jambo hilo.

“Sisi wanadamu tunapanga lakini Mungu naye anapanga yake, kazi ya Mungu haina makosa, tumshukuru kwa uhai na zawadi ya maisha yake, tutaendelea kumuombea na kuiweka familia yake kwenye maombi.

“Marehemu Dkt.Ndugulile ameweka heshima katika nchi yetu kwa kupata nafasi WHO, niseme kwamba Mungu amechukua amana yake lakini kwetu sisi ni kuendelea mbele tena kwenye ushindani wa nafasi hiyo,” amesema Rais Dkt.Samia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news