DAR-Watuhumiwa sita ambao ni Bato Bahati Tweve, Nelson Elmusa, Anitha Alfred Temba, Isaack Mwaifuani, Fredrick Juma Msatu, Benki Daniel Mwakalebela wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki jijini Dar es Salaam na kusomewa shtaka moja la jaribio la kumteka mfanyabiashara Deogratius Tarimo kinyume na sheria.
Akiwasomea shtaka hilo Wakili wa Serikali John Mwakifuna mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Ramadhan Rugemalira amesema, inadaiwa Novermber 11, 2024 eneo la Kiluvya Madukani Ling’wenye Kinondoni jijini Dar es Salaam washtakiwa hao wote kwa pamoja walijaribu kumteka mfanyabiashara Deogratius Tarimo kinyume na sheria.
Aidha,washatkiwa wote sita wameshindwa kukamilisha masharti ya dhamana na wamepelekwa rumande hadi Desemba 19, 2024 ambapo kesi hiyo itatajwa.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo