DAR- Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linawashikilia watuhumiwa wanne akiwemo Deogratius Paul Masawe (49) mkazi wa Tegeta kwa ndevu na Idd Bakari (30) mkazi Tegeta kwa Ndevu ambao wote ni Makuli, pia Omar Issa (47) Mpiga debe Mkazi wa Tegeta Dawasco na Rashid Mtonga (29) Dereva bodaboda Mkazi wa Bunju kwa tuhuma za kufanya mauaji ya Mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania aitwaye Amani Kamguna Simbayao pia kumjeruhi Adriano Fredrick wa TRA.
Taarifa iliyotolewa Desemba 7,2024 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne imeeleza kuwa,“Watuhumiwa hao na wengine ambao bado wanahojiwa kwa kina walikamatwa baada ya kuwashambulia Maafisa hao wa TRA wakati wakitekeleza majukumu yao ya kisheria, waliliharibu pia gari STL 9923 Toyota Land Cruiser mali ya Mamlaka ya Mapato Tanzania.”
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo