Magereza wamuonya Haji Manara kwa maneno yenye kutweza utu, kulifedhehesha jeshi

DAR-Kupitia ukurasa wa Instagram wa Jeshi la Magereza Tanzania limemuonya shabiki na mwanachama wa Yanga Sc, Haji Manara kwa kauli isiyo ya kiungwana aliyoitoa baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa jana kuanzia saa 10:00 jioni kwenye Dimba la KMC kati ya Yanga na Tanzania Prisons.
“Baada ya kumalizika kwa mchezo, Haji Manara alianza kuongea na Vyombo vya Habari akiwa ameegesha gari lake mbele ya gari la Jeshi la Magereza.

“Kwa kuwa alikuwa amezuia gari la Jeshi kuondoka, aliombwa atoe nafasi kwa kusogeza gari lake kuruhusu gari alilokuwa amelizuia liweze kupita na yeye aendelee na mahojiano yake.

“Hata hivyo, pamoja na kuombwa alikataa kwa dharau na kuanza kutoa maneno yasiyo ya kiungwana, yenye viashiria vya kutweza utu na yenye mwelekeo wa kulifedhehesha Jeshi la Magereza.

“Uongozi wa Jeshi unatoa onyo na kuwataka wananchi kuacha kutoa kauli zenye mwelekeo wa kubeza, kutweza, kudharau mamlaka yake au kulifedhehesha na kwamba halitasita kuchukuwa hatua kali kwa yeyote atakayehusika,” Taarifa ya Jeshi la Magereza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news