Mahafali Skuli ya Turkish Maarif yafana,Serikali yatoa wito kwa wanafunzi

ZANZIBAR-Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, ndugu Khamis Suleiman Mwalim amewahimiza wanafunzi kuwa na nidhamu pamoja na kuwa wazalendo wa kuipenda nchi yao.
Hayo ameyasema wakati wa Mahafali ya Nne ya wanafunzi wa kidato cha nne pamoja na darasa la saba katika Skuli ya Turkish Maarif iliyopo Mombasa.

Amesema, uzalendo husaidia kuimarisha kwa amani na utulivu jambo ambalo linasisitizwa na viongozi wa nchi.
Amesema,uzalendo ni pamoja na kuzijua nyimbo za Taifa pamoja kuelewa ujumbe uliopo ndani yake.

Aidha, amewasisitiza vijana hao kuzidi kufanya bidii zaidi katika masomo yao ili kuweza kufaulu na kutimiza malengo yao.
Katibu Khamis, amewaomba wazazi na walezi wa wanafunzi kufanya bidii katika malezi ya watoto pamoja na kuwakinga na matendo maovu ikiwemo ya udhalilishaji.

Naye Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo ndugu Ahmed Ali Makame amesema Skuli yao inaendelea kufanya vizuri kutoka mwaka hadi mwaka kutokana na ushirikiano mzuri baina ya wazazi na walezi wa wanafunzi.
Katika risala ya wanafunzi hao wamewashukuru walimu wao kwa kuwa pamoja nao na kuhakikisha wanafaulu na kufanya vizuri katika masomo yao.

Aidha, waliomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kuwasaidia katika vifaa vya maabara, vifaa vya kufundishia ikiwemo kompyuta pamoja na kupatiwa nafasi za masomo nje ya nchi.Jumla ya wanafunzi 144 wamemaliza masomo yao ya darasa la saba na kidato cha nne Ambapo kwa darasa la saba ni wanafunzi 82 wanaume 35 na wanawake 47 na kwa kidato cha nne ni wanafunzi 62 wanaume 20 na wanawake 42.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news