Makamu wa Pili wa Rais azindua Barabara ya Mwera-Polisi hadi Kibonde Mzungu

ZANZIBAR-Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema, kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya Mwera-Polisi hadi Kibonde Mzungu kutasaidia kukuwa kwa uchumi wa nchi pamoja na kuongezeka kwa thamani katika vijiji vilivyopitiwa na barabara hiyo.
Ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Barabara ya Mwera-Polisi - Kibonde Mzungu uliofanyika katika viwanja vya Mwera Polisi ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964.

Amesema, ukuaji wa uchumi katika nchi na kuwepo kwa maendeleo endelevu kunategemea uwepo wa miundombinu bora na imara inayojengwa na Serikali kwa maslahi mapana ya wananchi ikiwemo miundombinu ya barabara na mengineyo.
Makamu wa Pili wa Rais amesema, kila mwananchi ana wajibu wa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi za kuwaletea wananchi maendeleo ambapo katika sekta ya miundombinu ya Barabara jumla ya kilomita 897.2 zimejengwa kwa kiwango cha lami mijini na vijijini na kupitiliza agizo la Ilani ya Uchaguzi lililoitaka Serikali kujengwa kilomita 196.7 za barabara.

Naye Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi, Mhe.Dkt.Khalid Salum Muhammed amesema?Serikali ya Awamu ya Nane katika kuhakikisha Zanzibar inaimarika na kuzidi kupiga hatu kimaendeleo imedhamiria kujenga barabara zenye urefu wa zaidi kilomita 897.2 ambapo wananchi wa Jimbo la Mwera na Jimbo la Fuoni wamenufaika na ujenzi wa barabara ya Mwera - Kibonde Mzungu.

Akitoa taarifa ya kitaalamu juu ya ujenzi wa Barabara ya Mwera-Kibonde Mzungu, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiano na Uchukuzi,Dkt. Habiba Hassan Omar amesema, barabara hiyo yenye urefu wa Kilomita 6.1 iliyojengwa na Mkandarasi Kampuni ya Iris na kusimamiwa na Mshauri elekezi mzalendo kutoka Wakala wa Barabara Zanzibar (ZANROD) hadi kumalizika kwake imegharimu zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 80 ambazo gharama hizo ni fedha kutoka Serikalini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news