KIGOMA-Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema msimu ujao litatoza ada kwa makocha wa kigeni.
Sambamba na wasaidizi wao kama wanavyofanya kwa wachezaji wanaotoka nje ya Tanzania.
Rais wa Shirikisho hilo, Wallace Karia ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara (TPLB) mkoani Kigoma ambapo mpango huo utaanza msimu wa mwaka 2025/26.
Alisema sababu ya kufanya hivyo ni kudhibiti ubora wa makocha wa kigeni na wasaidizi wao kwani wamebaini baadhi yao hawana sifa hizo kuliko wazawa.
Pia, Karia aliongeza kuwa mpango huo utakuwa sehemu ya chanzo cha mapato kwa shirikisho hilo kama ambavyo wanapata kutokana na kutoza ada hizo kwa nyota wa kigeni.