ZANZIBAR-Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe. Mama Mariam Mwinyi ameizindua bodi na ofisi mpya ya taasisi anayoingoza ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF).
Uzinduzi wa bodi na ofisi hiyo umefanyika leo tarehe 5 Disemba 2024, Kilimani Mnara wa mbao Mkoa wa Mjini Magharibi ambako kwasasa ndio itakua ofisi itakayoratibu na kutekeleza shughuli zote za ZMBF nchini.
Aidha, uzinduzi wa bodi mpya ya “Zanzibar Maisha Bora Foundation” umekuja baada ya kumaliza muda wake bodi ya zamani ambayo Mama Mariam Mwinyi ameisifu kwa kazi kubwa waliyoifanya kwa ZMBF na jitihada waliyoweka hadi kuifanikisha taasisi hiyo kujivunia mafanikio makubwa iliyonayo sasa.
Mama Mariam Mwinyi ameeleza kazi ya Bodi hizo ni kusimamia, kushauri na kuiwekea malengo na kuujengea upeo pamoja na kuuongoza uongozi wa taasisi hiyo katika kuhakikisha inafanikisha malengo yake iliyojiwekea na kusimamia mpango mkakati wa taasisi hiyo.
Halikadhalika Mama Mariam Mwinyi, aliishukuru taasisi ya “Benjamin Mkapa Foundation” kwa msaada mkuwa walioutoa kwa “Zanzibar Maisha Bora Foundation” amesema taasisi hiyo imekua dada wa ZMBF kwa kila hatua ya mafanikio iliyopiga.
Bodi mpya ya “Zanzibar Maisha Bora Foundation” iliyozinduliwa rasmi itafanyakazi kwa mwaka 2024/2025 hadi 2026/2027.
Tags
Dkt.Hussein Ali Mwinyi
Habari
Mama Mariam Mwinyi
Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF)
Zanzibar News