PRETORIA-Klabu ya Mamelodi Sundowns imemsimamisha kocha wa timu ya wanawake, Jerry Tshabalala ili kupisha uchunguzi.
Ni kuhusu tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wasichana wa timu hiyo ambapo inadaiwa kocha huyo amekuwa akiingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo vya wasichana ikiwa wasichana wako uchi.
Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo, wachezaji wa timu hiyo wamemlalamikia kocha huyo kutamka matamshi yasiyofaa ikiwemo kuwauliza ni mara ngapi huwa wananyoa sehemu zao za siri.
“Ikitokea uchunguzi utabaini ukweli unaothibitisha kwamba hatua zichukuliwe, bodi itachukua hatua zinazofaa mara moja. Mamelodi Sundowns itatoa taarifa kwa wakati kuhusu matokeo ya uchunguzi huo na hatua zitakazochukuliwa.”