DAR-Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya kutengeneza magari ya umeme ya KAYPEE MOTORS ambaye pia ni GenC na mtangazaji kutoka Clouds Media Group, Ally Masoud Nyomwa maarufu kama Masoud Kipanya, ametunukiwa shahada ya udaktari wa heshima.
Shahada hiyo inatambua mchango wake kwenye jamii, ubunifu na ustahimilivu, ambayo inatambulika kama Vanguard Honorary Degree for Creativity, Resilience and Social Impact.