DODOMA-Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mheshimiwa Anthony Mavunde ametembelea Gereza Kuu Isanga akiambatana na wadau wa maendeleo Dodoma maarufu kama Dodoma Legends jana Desemba 28, 2024 na kupokewa na Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza (CP),Nicodemus Tenga kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania (CGP),Jeremiah Katungu.

Kamishna Nicodemus Tenga amemshukuru Mhe. Mavunde pamoja na wadau alio ambatana nao kwa kuamua kutembelea Gereza la Isanga na kutoa zawadi mbalimbali kwaajili ya matumizi ya Wafungwa na Mahabusu huku akisema hiyo ndio namna bora ya ushirikishwaji wa jamii katika dhana ya Urekebu wa wafungwa.

