Mchango wa Ushirika katika mafanikio ya Uhuru wa Tanganyika

DAR-Siku ya tarehe 9, Desemba 1961 ni siku ambayo Tanganyika ilijipatia uhuru wake kamili kutoka kwa Mkoloni, Tanganyika iliyokuwa inaongozwa na Koloni la Kiingereza chini ya Gavana Sir. Richard Gordon Turnbull ilianza mapambano yake ya kujitawala na kuwa huru toka enzi ya watawala machief ambao walipinga waziwazi uvamizi wa wakoloni katika milki za utawala wao.
Mapambano ya uhuru na kujitawala yalianza kupitia makundi mbalimbali ya kijamii, uchumi, Sanaa, michezo n.k makundi haya yalibainishwa kama ifuatavyo:

1. Umoja wa Vijana mfano TANU YOUTH LEAGUE

2. Umoja wa Wanawake

3. Vyama vya Wafanyakazi mfano TANGANYIKA AFRIKAN GOVERNMENT SERVANTS ASSOCIATION ( _TAGSA_ ) COMMERCIAL EMPLOYEES ASSOCIATION (CEA) nk

4. Chama cha Wazazi mfano TANGANYIKA PARENTS ASSOCIATION (TAPA)

5. Vyama vya Ushirika vilivyokuwa vimeenea Nchi nzima baada ya vita ya pili ya Dunia viliungana na TANU katika mapambano ya uhuru mfano VICTORIA FEDERATION COOPERATIVE UNION

6. Vilabu vya mpira wa miguu , mfano YOUNG AFRICAN SPORTS CLUB (Yanga) na SUNDERLAND (Sanda) simba ya sasa

7. Vyombo vya habari mfano SAUTI YA TANU na MWAFRIKA

Vyama vya Ushirika vilitoa viongozi makini waliosaidia upatikanaji wa uhuru na hata Mwalimu Nyerere kuthamini uwezo wao na kuwashirikisha katika Baraza lake la kwanza la Mawaziri la Tanganyika 1961 , viongozi hao ni pamoja na

1. Nsilo Swai WAZIRI WA BIASHARA NA VIWANDA

2. Paul Bomani WAZIRI WA KILIMO

3. George Kahama WAZIRI WA MAMBO YA NDANI

(Building a peaceful Nation- PAUL BJERK ).

Ukifanya tathmini kwa idadi ya Mawaziri wa Baraza la kwanza la Tanganyika huru 1961 utagundua robo (1/4) ya mawaziri walikuwa wametokana na Ushirika, kati ya wizara 11 zilizoundwa Wizara 3 ziliongozwa na watu makini kutoka kundi la wanaushirika

Tunapokwenda kusheherekea Siku ya Uhuru tarehe 9 Desemba, 2024 tunapaswa kukumbuka mchango wa Ushirika wa hali, mali, rasilimali watu n.k, ni muhimu sana kuzingatia uendelevu wa Ushirika wa Sasa ili kuenzi matunda ya UHURU WETU.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news