GEITA-Mchekeshaji maarufu wa mitandao ya kijamii nchini mtoto Frank Patrick maarufu kwa jina Molingo (17) mkazi wa Wilaya ya Chato mkoani Geita amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Ni baada ya kusumbuliwa na tatizo la kupungukiwa damu mara kwa mara pamoja na kuvimba miguu huku ikitajwa kuwa kifo hicho ni pigo kubwa kwa wasanii wachanga wanaochipukia katika sanaa ya vichekesho.
Mlezi wa msanii huyo ambaye alikuwa akimrekodi vichekesho na kuvisambaza mitandaoni Muddy Msomali amethibitisha taarifa hizo.