DAR-Aliyekuwa Mhasibu wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC FC), Bw. Atulinga Barongo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni jijini Dar es Salaam na kufunguliwa shauri la uhujumu uchumi Namba 33404/2024.
Katika shauri hili, Bw. Barongo anashtakiwa kwa kufanya ubadhirifu wa fedha kiasi cha shilingi 8,910,000 kinyume na kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 kama ilivyorejewa mwaka 2019.
Pia ameshtakiwa kwa kosa la kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri wake kinyume na kifungu cha 22 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na rushwa Sura ya 329 Rejeo la 2019.
Mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka na Mwendesha Mashitaka wa TAKUKURU Wakili Aidan Samali na shauri hili linasikilizwa na Mh. Hakimu Josiah.
Shauri hili limepangwa kuanza kusikilizwa hoja za awali (PH) tarehe 19 Desemba,2024.
Tags
Habari
Kinondoni Manispaa
Michezo
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
TAKUKURU Tanzania