SIMIYU-Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Kassim Majaliwa leo Desemba 22, 2024 ni Mgeni Rasmi kwenye mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Jimbo Busega, unaofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Simba wa Yuda, Wilaya ya Busega mkoani Simiyu.