Mifumo imara ya Mahakama ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi-Waziri Mkuu

NA MARY GWERA
Mahakama Arusha

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amesema kuwa mifumo imara ya Mahakama katika utoaji wa haki ni muhimu na ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akifungua Mkutano Mkuu wa 21 wa Chama cha Mahakimu na Majaji wa Afrika Mashariki (EAMJA) leo tarehe 03 Desemba, 2024 katika Hoteli ya Gran Melia` jijini Arusha.

Mhe. Majaliwa ameyasema hayo leo tarehe 03 Desemba, 2024 kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 21 wa Chama cha Mahakimu na Majaji wa Afrika Mashariki (EAMJA) unaofanyika katika Hoteli ya Gran Melia` jijini Arusha.

“Mfumo ulioimarishwa wa utoaji wa haki ndani ya Mahakama ni muhimu kwa ujumuishaji wa kina wa kikanda na ukuaji wa uchumi, nikiwa kama mmoja wa viongozi katika ukanda huu, ninathamini sana mikusanyiko ya kikanda kama hii, ambayo huwaleta pamoja Mahakimu na Majaji wa Afrika Mashariki kushughulikia masuala muhimu ya kitaifa na kikanda yanayolenga kutoa haki na hatimaye kukuza uchumi wa ukanda huu,” amesema Waziri Mkuu.

Aidha, amepongeza Viongozi wa Chama cha Mahakimu na Majaji wa Afrika kwa kuchagua Kaulimbiu isemayo, ‘Uboreshaji wa mifumo ya utoaji haki kwa ajili ya kuimarisha utengamano na Ukuzaji Uchumi katika Ukanda wa Afrika Mashariki’ kwa kuwa inahimiza ustawi wa haki kwa wananchi ambao unaleta amani na utulivu na hatimaye kukuza uchumi.
Sehemu ya Majaji wa Mahakama ya Rufani pamoja na washiriki wengine wa Mkutano Mkuu wa 21 wa Chama cha Mahakimu na Majaji wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Mgeni Rasmi, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (hayupo katika picha) alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema kusanyiko hilo litatoa fursa ya kuchanganua changamoto zinazoukabili ukanda huo katika kutoa haki na kuandaa mikakati ya kukabiliana nazo na kwamba mwavuli wa EAMJA unawawezesha kushirikiana katika kuhakikisha haki yenye ufanisi na shirikishi kwa wananchi wa ukanda huo.

Ameongeza kuwa, nchini Tanzania, chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kumefanyika uamuzi muhimu ya kisera ya kijamii na kiuchumi ambayo yanajenga muelekeo wa maendeleo, yenye lengo la kuboresha ustawi na ustawi wa watu wa Tanzania.

“Sera hizi ni pamoja na, miongoni mwa nyingine, kuzingatia kuimarisha uwezo wa kitaasisi ndani ya mfumo wa utoaji haki kwa njia ya kisasa. Lengo ni kukuza haki za kimsingi za mtu binafsi, kuimarisha mchango wa Mahakama katika mazingira mazuri ya uwekezaji, na kuboresha utumiaji wa teknolojia za kisasa ili kusaidia Mahakama inayozingatia raia, inayohakikisha utoaji wa haki kwa ufanisi, uwazi na kwa wakati,” ameeleza Mhe. Majaliwa.

Ameongeza kwamba, Serikali ya Tanzania inaiheshimu Mahakama na inaunga mkono kikamilifu juhudi zake za kuwezesha mfumo wa utoaji haki kuwa wa kisasa.

“Serikali yetu inaamini kuwa upatikanaji wa haki ni nguzo ya msingi inayosukuma mbele malengo ya Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025 na Lengo la Maendeleo Endelevu namba 16, ambalo linajitolea kukuza jamii zenye amani na ushirikishi kwa maendeleo endelevu, kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wote, na kujenga taasisi zenye ufanisi, zinazowajibika katika ngazi zote," amesisitiza Waziri Mkuu.

Kadhalika, Mgeni Rasmi huyo amesema kwamba, utoaji haki ni muhimu kwa kuzingatia utawala wa sheria, utawala bora na uhuru wa mahakama, ambayo yote yanachangia ukuaji wa uchumi.

“Kupitia Mipango yetu ya Maendeleo ya Miaka Mitano, Serikali ya Tanzania imedhihirisha dhamira yake ya kuboresha mfumo wa utoaji haki. Mnamo 2023, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan aliteua "Tume ya Rais" ya watu mashuhuri kuchunguza mageuzi katika mfumo wa haki za jinai,” ameeleza Mhe. Majaliwa.

Waziri Mkuu amewakumbusha Majaji na Mahakimu wa Ukanda wa Afrika Mashariki kuhusu matumizi ya teknolojia kuwa ni muhimu kuzingatiwa kwa kufikia utoaji wa haki wenye ufanisi.

Kwa upande wake, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amesema Mhe. Prof. Kabudi amesema, Majaji na Mahakimu na watu muhimu wenye kuchangia amani na utulivu wa watu na nchi kwa ujumla.

“Mtu yeyote anahitaji kupata haki yake, sehemu anayokimbilia ni Mahakama kutafuta haki, hivyo wananchi wanawaamini ninyi na wana imani kuwa wanapokuja kwenu wanajua watapata haki zao, hivyo ni muhimu kuilinda imani hii kwa kutekeleza kile ambacho mmekasimiwa kwa mujibu wa sheria,” amesema Mhe. Prof. Kabudi.

Serikali ya Tanzania inathamini kile kinachofanywa na EAMJA na kwamba kufanyika kwa Mkutano huu nchini Tanzania ni dhahiri kuwa kutokana na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Nchi wanachama wa Afrika Mashariki.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani (kushoto) pamoja na washiriki wengine wa Mkutano Mkuu wa 21 wa Chama cha Mahakimu na Majaji wa Afrika Mashariki (EAMJA) wakiwa katika hafla ya ufunguzi wa mkutano huo leo tarehe 03 Desemba, 2024 jijini Arusha.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Manyara na Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT), Mhe. John Rugalema Kahyoza (kushoto) pamoja na washiriki wengine wa Mkutano Mkuu wa 21 wa Chama cha Mahakimu na Majaji wa Afrika Mashariki (EAMJA) wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Mkutano huo leo tarehe 03 Desemba, 2024.
Picha mbalimbali za Washiriki wa Mkutano wa 21 wa EAMJA wakifuatilia kinachojiri.
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya (kulia) pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) wakiwa katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 21 wa Chama cha Mahakimu na Majaji wa Afrika Mashariki (EAMJA) leo tarehe 03 Desemba, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Gran Melia' jijini Arusha.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mahkama ya Zanzibar, Bw. Khai Mbarouk (anayefuata) pamoja na washiriki wengine wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 21 wa Chama cha Mahakimu na Majaji wa Afrika Mashariki (EAMJA).
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 21 wa Chama cha Mahakimu na Majaji wa Afrika Mashariki (EAMJA) leo tarehe 03 Desemba, 2024 katika Hoteli ya Gran Melia` jijini Arusha.
Meza kuu wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (hayupo katika picha).

Amepongeza pia Kaulimbiu iliyochaguliwa na kueleza kwamba, Wizara itatekeleza yote yatakayoelekezwa na kuazimiwa katika Mkutano huo lengo likiwa ni kuendelea kuboresha huduma ya utoaji haki kwa wananchi.

Mkutano huo umekutanisha zaidi ya wajumbe 387 kutoka Zanzibar, Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi na Sudani ya Kusini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news