Mikoa mitano yauza korosho za shilingi trilioni 1.44 kwa mwaka 2024/2025

NA AHMAD MMOW
Lindi

WAKATI msimu wa ununuzi wa korosho kwa mwaka 2024/2025 ukikaribia kumalizika. Mpaka sasa tani 401,000 za korosho zenye thamani ya shilingi 1.44 trilioni zimenunuliwa.
Akizungumza kwenye mnada wa kumi wa Chama Kikuu cha Ushirika cha RUNALI kwa msimu wa 2024/2025 uliofanyika mjini Nachingwea, ofisa usimamizi wa fedha wa Soko la Bidhaa Tanzania(TMX), Prince Mng'ong'o alisema hadi kufikia sasa takribani tani 401,000 za korosho ghafi zenye thamani ya takribani shilingi trilioni 1.44 zimeuzwa na kununuliwa.

Mng'ongo amesema hadi sasa chama kikuu cha RUNALI kimefanikiwa kuuza tani 70,360 kati ya tani hizo 401,000 zilizozalishwa na mikoa yote mitano inayolima zao hilo kwa wingi hapa nchini.

Ofisa huyo wa TMX amesema mbali na korosho taasisi hiyo imeweza kusimamia mauzo kupitia minada zao la kakao. 

Akiweka wazi kwamba hadi sasa takribani tani 11,000 zenye thamani ya shilingi bilioni 210 zimeuzwa na kununuliwa.
"Lakini pia TMX imeendesha minada ya madini. Tayari mpaka sasa zimeuzwa gramu 610,000 ambazo sawa na kilo 610 zenye thamani ya shilingi bilioni 610 kwa njia ya soko la bidhaa Tanzania. 

"Mkakati ni kwamba ifikapo mwaka 2025 mazao yote ya kimkakati yauzwe kwa mfumo wa TMX," alibainisha Mng'ong'o.

Chama kikuu cha RUNALI kilichopo mkoani Lindi kinatarajia kufanya mnada mmoja wa mwisho. 

Ambapo kwa mujibu wa Mng'ong'o baadhi ya vyama vikuu vya ushirika tayari vimefunga msimu wa ununuzi kwa mwaka 2024/2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news