Mkutano wa Kimataifa wa Chama cha Majaji na Mahakimu Afrika Mashariki waanza jijini Arusha

NA FAUSTINE KAPAMA
Mahakama Arusha

MKUTANO Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu kutoka Nchi za Afrika Mashariki unaofanyika jijini Arusha, kuwaleta pamoja zaidi ya washiriki 300 kutoka Ukanda huo, umeanza leo tarehe 2 Desemba, 2024.
Kikao cha Baraza Tendaji la Chama cha Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki kikianza sara na wajumbe kuimba wimbo wa Afrika Mashariki.
Kikao cha Baraza Tendaji la Chama cha Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki kinaendelea huku Viongozi wakuu wakifuatilia kinachojiri.
Kikao kinaendelea huku wajumbe (juu na picha mbili chini) wakifuatilia yanayotokea.
Mapema asubuhi kimefanyika kikao cha Baraza Tendaji la Chama cha Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki kujadili mambo mbalimbali ya kiutendaji, changamoto na mafanikio lukuki ambayo tayari yameshapatikana.

Kikao pia kimetoa taswira halisi kuhusu ushiriki wa wanachama kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka na mambo mbalimbali yatakayofanyika kwa kipindi cha takribani siku tano.

Mada mbalimbali zitajadiliwa wakati wa Mkutano, ikiwemo Kuimarisha Msingi wa Mahakama: Mahakama kama Msingi wa Mnyororo wa Haki Jinai, Maboresho katika Kuimarisha Utoaji wa Haki; Uoanishaji Sheria za Kazi Afrika Mashariki ili Kuboresha Utatuzi wa Migogoro; Wajibu wa Mifumo ya Kielektroniki ya Usimamizi wa Mashauri katika Kuboresha Ufanisi wa Mahakama na Uamuzi wa Makosa Yasiyo na Mipaka katika Mahakama za Afrika Mashariki: Mfumo na Changamoto za Kisheria.
Viongozi wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania wakitambulishwa mbele ya Baraza Tendaji la Chama cha Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki.
Viongozi wakuu wa Baraza Tendaji la Chama cha Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye picha ya pamoja. Picha mbili chini ni Viongozi wengine wa Baraza hilo waliohudhuria Kikao hicho.
Wajumbe wa Baraza wakiwa katika picha ya pamoja.

Jaji Mkuu wa Tanzania Mstaafu, Mhe. Mohamed Chande Othman na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri, Bi. Suzanne Ndomba ni miongoni mwa Wataalamu wa Sheria watakaochokoza mada kwenye Mkutano huo, huku Mhadhiri Nguli wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Shule ya Sheria kwa Videndo, Prof. Hamudi Ismail Majamba akiwa mmoja wa waongoza Majopo kujadili mada hizo.

Watanzania wengine watakaoshiriki kwenye Majopo kujadili mada hizo ni Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar, Mhe. Khadija Shamte Mzee, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Aisha Sinde na Mkurugenzi wa Menejimenti ya Mashauri, Mhe. Desdery Kamugisha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news