MBEYA-Disemba 11, 2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Mbeya mbele ya Hakimu Mkazi,Mhe. Happynes Chuwa limefunguliwa Shauri la Jinai Namba 34527/2024 kati ya Jamhuri dhidi ya Nelusigwe Enock Kajuni ambaye ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwakibete.
Kajuni anashtakiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi kinyume na kifungu cha 96(1) na (2) cha kanuni ya adhabu.
Akisoma hati ya Mashtaka, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),Emmanuel Jilugu amesema,mshtakiwa huyo alitenda kosa kwa kumfukuza kazi Mwalimu Sipola Shadrack Mwaisabila.
Sipola alikuwa ni mwalimu wa ajira ya mkataba wa muda mfupi ambapo alifanya hivyo pasipo kufuata taratibu za kiutawala.
Mshtakiwa amekana shitaka na amedhaminiwa hadi Desemba 17,2024 shauri litakapokuja kwa hatua kusoma maelezo ya awali.
Tags
Habari
Mahakamani Leo
Manispaa ya Ubungo
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
TAKUKURU Tanzania