DODOMA-Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari amekutana na kufanya kikao na Wataalamu kutoka Shirika la Maendeleo la Uingereza (FCDO-UK) ambao ni wafadhili wa mradi wa BSAAT.
Lengo la Kikao hicho ni kufanya Tathimini ya utekelezaji wa shughuli za Mradi wa Mfumo endelevu wa Kupambana na Rushwa Tanzania (BSAAT) kwa Mwaka 2024.