DAR-Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari amehudhuria sherehe za kuapishwa kwa Mawakili wapya 524 wa Kujitegemea, zilizofanyika tarehe 12 Desemba, 2024 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.Akizungumza wakati wa sherehe hizo za kuapishwa kwa Mawakili wa Kujitegemea, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amewataka Mawakili hao kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia miiko yao.
"Nawaomba mfanye kazi kwa kuzingatia weledi, maadili, na taratibu zinazowaongoza Mawakili wa Kujitegemea,"amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Aidha, Mhe. Johari amewakumbusha Mawakili wa Kujitegemea waendelee kusoma na kujifunza ili waendane na kasi na kusaidia kufikia Dira ya Taifa ya 2050 iliyozinduliwa hivi karibuni.
Mgeni rasmi katika sherehe hizo za uapisho wa Mawakili wa Kujitegemea ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma.