PWANI-Mwekezaji mzawa, Keneth Amon anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Pwani kwa tuhuma za kuwajeruhi wafugaji wanne.
Ni kwa kutumia bunduki aina ya shotgani baada ya mifugo yao kuingia katika shamba lake.
Tukio hilo lilitokea Desemba 2, 2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Hayo yamebainishwa leo Desemba 5,2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salim Morcase wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake Kibaha.
“Vurugu zilitokea kati ya wafugaji na walinzi wa shamba, na baada ya Keneth kutoka nje, alijitokeza kwa bunduki na kuwajeruhi wafugaji wanne."
Kamanda huyo amesma, wafugaji hao walikimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Amesema,Keneth Amon anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi na atafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.