Mwenyekiti wa RUNALI awatahadharisha viongozi na watendaji wa AMCOS

NA AHMAD MMOW
Nachingwea

VIONGOZI watendaji wa vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) vilivyopo katika wilaya za Liwale, Ruangwa na Nachingwea wameaswa wawe makini katika kipindi hiki ambacho msimu wa ununuzi wa korosho unaelekea kufika tamati.
Tahadhari hiyo imetolewa leo mjini Nachingwea na mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika cha RUNALI, Audax Mpunga mara baada ya kukamilika mnada wa kumi wa zao la korosho kwa chama hicho kwa msimu wa 2024/2025 ambao ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa chama hicho.

Mpunga alisema wakati msimu wa ununuzi wa korosho unakaribia kumalizika viongozi na watendaji wa AMCOS zilizo chini ya RUNALI wawe makini ili wasipate matatizo.

"Korosho hazijawahi kumuacha mtu salama. Angalieni umbo la korosho zenyewe matajua hazimuachi mtu salama, maana zimepinda," alionya Mpunga.

Mwenyekiti huyo alibainisha kwamba mwisho wa misimu baadhi ya viongozi na watendaji hutumia kujinufaisha kwa kuruhusu na kupokea korosho chafu na mambo mengine yasiyokubalika. Kwahiyo wasithubutu kufanya hivyo. Kwani serikali ipo makini na inafuatilia kila hatua.

Ameweka wazi kwamba vyama vikuu vingi vya ushirika ambavyo maeneo yake yanazalisha korosho vimefunga msimu wa ununuzi. Kwahiyo ni rahisi korosho zisizo na ubora kuletwa na kuingizwa kwenye mauzo kwenye vyama ambavyo bado havijafunga msimu. Ikiwamo chama kikuu cha ushirika cha RUNALI.

Aidha, Mpunga amewahakikishia wakulima kwamba hakutakuwa na changamoto ya vifungashio. Kwani tayari wilaya za Liwale na Ruangwa zimepata gunia 3000 kila wilaya ikiwa ni kati ya gunia 22,000 zinazotarajiwa kupata chama hicho. 

Ambapo wilaya ya Nachingwea itapata baada ya kuwasili mzigo uliosalia. Kwani tayari kiasi kilichosalia kinatarajiwa kufika wakati wowote toka sasa.

Katika mnada huo jumla ya tani 2,728 na kilo 19. Ambapo korosho zenye ubora wa daraja la kwanza zilikuwa tani 2,398. Wakati korosho zenye ubora wa daraja la pili zilikuwa tani 330 na kilo 224.

Bei ya juu ya korosho za daraja la kwanza ilikuwa shilingi 2,200. Na bei ya chini ilikuwa shilingi 2,010 kwa kila kilo moja. Ambapo korosho zenye ubora wa daraja la pili zilinunuliwa kwa bei ya juu ya shilingi 1,840 na bei ya chini shilingi 1,780. Korosho zote zimenunuliwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news