Mwinjilisti Temba aibua hoja nzito uchaguzi wa Serikali za Mitaa

DAR-Mwinjilisti wa Kimataifa, Alphonce Temba amesema, haoni tija ya kuwa na uchaguzi wa viongozi ngazi ya mitaa, vijiji na vitongoji kwani majukumu yao yanafanywa na mabalozi wa nyumba 10 nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Desemba 1, 2024 jijini Dar es Salaam, Mwinjilisti Temba amesema, kufanya uchaguzi wa viongozi hao ni matumizi mabaya ya fedha kwa sababu baada ya kuchaguliwa hawana majukumu ya kufanya zaidi ya kuchangia migogoro hususani ya ardhi.

Mwinjilisti Temba amesema,imefika wakati kwa Serikali na Bunge kuangalia upya mfumo wa sasa wa kisiasa wa kuwa na mlundikano wa viongozi zaidi ya 10 wa kisiasa kama unatufaa kwa Wakati huu.

"Tuna viongozi wa kisiasa zaidi ya 10, je mfumo huu unatufaa kwa Wakati huu?. Tuna Balozi, Mwenyekiti wa Kitongoji, Kijiji, Mtaa na wajumbe watano, madiwani, Wabunge na kadhalika. Je kwa sasa kuna mahitaji ya kuwa na viongozi hawa?.

"Balozi anaweza na anatoshereza kuwa mwanagalizi wa Wananchi ngazi ya chini na kwasasa ni mabalozi wa nyumba hamsini, hamsini na wanafanya kazi nzuri sana. 

"Kazi ambazo tunajua zinafanywa na Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na Mitaa zinafanywa na mabalozi. Je hawa wengine (Wenyeviti wa Vitongoji, Vijiji na Mitaa) wanafanya kazi gani.

"Hawa viongozi wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji ndiyo wamekuwa wakileta migogoro ya ardhi Kwa wananchi, wao wamekuwa wakionekana kwenye kuuza maeneo."

Mwinjilisti Temba amesisitiza kuwa, viongozi hao wa Vijiji, Vitongoji na Mitaa hawana kazi ya kufanya ndiyo maana hata wamepokonywa mihuri na kukabidhiwa mabalozi.

Pia ametumia fursa hiyo kulaani mauaji yanayodaiwa kusababishwa na chaguzi hizi, akieleza kuwa vitendo hivi ni kujitakia laana zitakazotafuna hadi kizazi cha baadaye kwa muhusika wa vitendo hivyo.

Mwinjilisti Temba amesema kuwa,sio jambo la busara Kwa viongozi wa dini kukaa kimya vitendo hivyo vinapotokea,ambapo ameunga mkono kauli ya kukemea vitendo hivyo ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam,Askofu Jude Ruwa'ichi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news