DAR-Mwinjilisti wa Kimataifa,Alphonce Temba ametoa shilingi laki tano(500,000/=) kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili kukiwezesha kufanya uchaguzi wa viongozi utakaofanyika mwezi Januari 2025.
Akizungumza wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari uliyofanyika mwishoni mwa wiki Mwinjiristi Temba amesema kuwa yupo tayari kuongeza fedha zingine endapo viongozi wa CHADEMA waliopo madarakani kwa sasa watahitaji kwa ajili ya kufanikisha uchaguzi wao.
Kwa mujibu wa Mwinjilisti Temba fedha hizo zitakabidhiwa kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Jonh Mnyika hivi karibuni kwa lengo la kufanikisha uchaguzi huo na kudumisha amani kwa Taifa kwani CHADEMA ni chama kikuu cha Upinzani Nchini.
Aidha, amefafanua kuhusu fedha hizo nakusema kuwa yeye si yo mwanachama wa chadema,hivyo amemuomba Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika kuzipokea kwa ajili ya mkutano huo, na sababu kubwa ni kutokana na Chadema kuwa chama Kikuu cha Upinzani Tanzania nakwamba endapo akipatikana Mwenyekiti mwenye mihemuko na kigeugeu ataliingiza taifa katika Machafuko kwa misimamo yake akitolea mfano wa kipindi Chadema ilivyohamasisha Ukuta nchi nzima na hali kuwa mbaya hadi viongozi wa dini kuingilia kati,ambapo msimamo wa Lisu ulikuwa mkali sana lakini kwa busara za Mwenyekiti Mbowe aliwasikiliza viongozi wa dini na kulimaliza jambo hilo.
Aidha Mwinjilisti Temba amekishauri Chadema kuwa mfumo wa kuweka vikomo katika nafasi ya uwenyekiti taifa ni mfumo wa vyama Tawala, vyama vya upinzani vyote walioshinda urais ni wenyeviti au viongozi waliogombea kwa muda mrefu wakiwepo Marais wa Zambia, Michael Sara na Rais wa sasa Akainde na Malawi Rais Chakwera ambao wameomba zaidi ya Mara tano.
Aidha amekisihi chama hicho kuhakikisha kinachagua viongozi wa ngazi ya Taifa ambao wana maono makubwa ya kukiwezesha kushika dola ,pamoja na kulinda amani ndani na nje ya chama hicho.
"Wajumbe watakoshiriki uchaguzi huo wahakikishe wanachagua kiongozi ambaye ana uwezo wa kuongoza kwa kuwa na maono yatakayokifanya chama kipige hatua kubwa kutoka kilipo sasa na hata kushika dola,pamoja na kuhakikisha kuna amani ndani ya chama na Taifa kwa ujumla," amesema Temba.
Aidha, amemuonya mgombea wa nafasi ya uenyekiti Taifa aliyetangaza hivi karibuni kuwania nafasi hiyo Bw. Tundu Lisu kuacha kutoa maneno ya kejeli kwa mwenyekiti aliyopo madarakani kwa sasa Freeman Mbowe kwa kusema kuwa hana uwezo tena wa kukiongoza chama hicho.
"Namshangaa Tundu Lisu kwa maneno anayotoa ya kubeza uongozi wa Mbowe,hakumbuki kwamba Mbowe ndiyo aliyemshikia drip ya damu hadi Nairobi Kenya wakati aliposhambuliwa kwa kupigwa risasi"?alihoji Temba mbele ya waandishi wa habari.
Katika hatua nyingine Mchungaji huyo wa Kimataifa amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utendaji wake mzuri kutokana na kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji,nakukuza diplomasia ya kiuchumi.
Aidha, amesema kwamba 4R za Dkt Samia zimeleta matumaini makubwa ya kidemokrasia kwa Vyama vya siasa nakwamba hatua hiyo imeimarisha ushirikiano mzuri wa vyama hivyo.
Aidha,ikumbukwe kuwa,Lissu alivyopigwa risasi alikimbizwa katika Hospitali ya Dodoma, baadaye serikali ilitakakumwamishia Muhimbili,lakini Mheshimiwa Mbowe alipambana na kuzuia hivyo kutafuta chopa iliyompeleka Nairobi kwa hofu ya usalama wake.
Vilevile,Mbowe aliongoza uchangishaji na mamilioni ya pesa yakapatikana kwa ajili ya kumnusuru uhai wake.
"Kwa mtu mwenye fadhila hata kama anataka uongozi kwanza angetumia lugha nzuri kwa kujua chama kiliacha kila kitu kikampambania mke wake na familia walikichagua chama kiwe mstari wa mbele kuyaokoa maisha yake pamoja na ukweli Mungu aliusika kuokoa roho yake kupitia Chadema.
"Hata hivyo,Lissu amekuwa akivurugwa na watanzania waishio nje ya nchi ambao wengi wao wanatumia mitandao ya kimataifa kutukana nchi kwa matakwa yao ya mambo ya uraia pacha,waliwahi kufungua kesi nchini bila mafanikio yoyote."