Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha ateta na Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA)

NA JOSEPHINE MAJURA
WF

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, kwa niaba ya Katibu Mkuu, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), Dkt. Zelia Njeza, katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (Katikati), akikabidhiwa tuzo ya shukrani na Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), Dkt. Zelia Njeza (Kushoto) kwa niaba ya Katibu Mkuu, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, kwa mchango wake katika kufanikisha Mkutano wa 10 wa Wakaguzi wa Ndani Barani Afrika na kusaidia ukuaji wa kada ya ukaguzi wa ndani, walipokutana na kufanya mazungumzo, katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma. Kulia ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali (IAG), Bw. Benjamin Magai.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akiongoza mazungumzo kwa niaba ya Katibu Mkuu, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), Dkt. Zelia Njeza (hayupo pichani), katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma, kuhusu namna bora ya kushirikiana katika kukuza taaluma ya Wakaguzi wa ndani nchini. Kikao kilichohudhuriwa na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali (IAG), Bw. Benjamin Magai, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), Bw. Seif Hassan na Afisa Mikakati na Maendeleo ya Biashara wa Taasisi hiyo, Bi. Iq-lima Issa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akizungumza jambo kwa niaba ya Katibu Mkuu, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), Dkt. Zelia Njeza (hayupo pichani), katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma, kuhusu namna bora ya kushirikiana katika kukuza taaluma ya Wakaguzi wa Ndani nchini. Kikao kilichohudhuriwa na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali (IAG), Bw. Benjamin Magai (hayupo pichani), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), Bw. Seif Hassan (hayupo pichani) na Afisa Mikakati na Maendeleo ya Biashara wa Taasisi hiyo, Bi. Iq-lima Issa.
Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali (IAG), Bw. Benjamin Magai, akizungumza jambo wakati wa kikao cha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (hayupo pichani), kwa niaba ya Katibu Mkuu, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), Dkt. Zelia Njeza (hayupo pichani), katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma, ambapo walijadiliana namna bora ya kushirikiana katika kukuza taaluma ya Wakaguzi wa Ndani nchini.
Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), Dkt. Zelia Njeza, akisaini kitabu cha wageni wakati alipofika katika ofisi ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Bi. Amina Khamis Shaaban (hayupo pichani), Treasury Square, jijini Dodoma, kufanya mazungumzo kuhusu namna bora ya kushirikiana katika kukuza taaluma ya Wakaguzi wa ndani nchini, ambapo Kikao hicho kilihudhuriwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali (IAG), Bw. Benjamin Magai (hayupo pichani), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), Bw. Seif Hassan (hayupo pichani), na Afisa Mikakati na Maendeleo ya Biashara wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), Bi. Iq-lima Issa (hayupo pichani).
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Bi. Amina Khamis Shaaban (Katikati), Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), Dkt. Zelia Njeza (wapili kushoto), Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali (IAG), Bw. Benjamin Magai (wa kwanza kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), Bw. Seif Hassan (wa kwanza kushoto) na Afisa Mikakati na Maendeleo ya Biashara wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), Bi. Iq-lima Issa (wa pili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa kikao kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma, ambapo walijadiliana kuhusu namna bora ya kushirikiana katika kukuza taaluma ya Wakaguzi wa ndani nchini.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma).

Katika kikao hicho wamejadiliana namna bora ya kushirikiana katika kukuza taaluma ya Wakaguzi wa Ndani nchini, ambapo kikao hicho kimehudhuriwa pia na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali (IAG), Bw. Benjamin Magai na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), Bw. Seif Hassan na Afisa Mikakati na Maendeleo ya Biashara wa Taasisi hiyo, Bi. Iq-lima Issa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news