DODOMA-Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Samwel Maneno amewahimiza Mawakili wa Serikali kujisajili kwenye Mfumo wa Kidijitali wa OAG - MIS unaosimamiwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili waweze kurahisisha utendaji kazi wao.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameyasema hayo wakati akizungumza katika kikao kazi cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wakurugenzi wa Divisheni/Idara na Wakuu wa Vitengo vya huduma za Sheria Serikalini, kilichofanyika tarehe 06 Desemba, 2024 Jijini Dodoma.
"Nawasisitiza Mawakili wote wa Serikali kujisajili kwenye mfumo wa OAG - MISS, mfumo huu kwasasa umeboreshwa na una kila kitu ambacho Mawakili wa Serikali tunakihitaji kukipata,"alisema Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.