TANGA-Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Dennis L. Londo (Mb) ameeleza kuwa,Serikalil imejipanga kuzisimamia na kuziwezesha Halmashauri hususan za mipakani kuwa kiungo muhimu kwenye masuala ya mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hasa kuwawezesha wananchi kunufaika na fursa za Mtangamano.

Ziara hiyo ililenga kuangalia utekelezaji wa shughuli za Himaya Moja ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na hali ya miundombinu na uendeshaji wa OSBP hiyo.
Katika ziara hiyo, Mhe. Londo amepata fursa ya kuzungumza na Wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali zinazotoahuduma katika OSBP na kutoa wito kufanya kwa uadilifu na weledi ili kutimiza azma ya Serikali ya kuhamasisha mtanngmano kwa lengo la kukuza muingiliano na bishara za mipakani.
Mhe. Londo ameahidi Serikali itaendelea kutatua changamoto za kiuendeshaji zinaozikabili OSBP hiyo pamoja na changamoto wanazokutana nazo wafanyabiashara katika mpaka huo na mingine nchini.
"Jumuiya ina fursa nyingi ambazo hazijatumika ipasavyo kwa manufaa ya wafanyabiashara wetu na kuzitaka halmashauri kubuni mbinu na mikakati ya makusudi kuwawezesha Wafanyabiashara hususan wadogo kuongeza thamani ya bidhaa zao ili ziweze kuuzwa bila vikwazo katika nchi za jumuiya,"Mhe. Londo alisema.
