Naibu Waziri Mwinjuma aridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa viwanja vya mazoezi CHAN

DAR-Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma amesema kuwa ameridhika na maendeleo ya ujenzi wa kiwanja cha mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya Mashindano ya Wachezaji wa Ndani (CHAN) ambayo yanatarajiwa kufanyika Februari 2025 nchini Tanzania, Kenya, na Uganda.
Mhe. Mwinjuma amebainisha hayo alipotembelea eneo Gymkana jijini Dar es salaam kujionea maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo wa mazoezi wa Gymkhana ambapo amesema Tanzania ipo tayari kwa mshindano hayo huku akisisitiza kuwa ujenzi wa viwanja vya Gymkhana na Shule ya Sheria umefikia asilimia 50.
"Mkandarasi wakati anaingia mkataba huu ambao ulikuwa unakwenda kukarabati viwanja hivi vitatu vya mazoezi ilikuwa vikamilke mwishoni mwa mwezi January, tumekubaliana kwamba vitakuwa vimekamilika Januari 21, nimemuomba kama kuna mambo tunaweza kuyaharakisha kabla ya Januari 21 itakuwa vizuri,” Mhe. Mwinjuma amesema.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mtendaji wa Suma JKT, Kanali Shija Rupi, amesema wanaendelea kutekeleza maagizo na kuhakikisha viwanja vinakidhi viwango vya CAF.

"Maandalizi yanaendelea na Mheshimiwa Naibu Waziri amejionea jitihada tunazofanya. Tunatarajia kukamilisha ujenzi na kukabidhi ifikapo Januari 21, 2025," amesema Rupi.
Ziara hiyo inatarajiwa kuendelea kesho katika uwanja wa Jenerali Meja Isamuhyo pamoja na Shule ya Sheria ili kujionea maendeleo ya ujenzi na kuhakikisha kila kitu kinakuwa kimekamilika kuelekea kwenye mashindano makubwa yanayokuja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news