Namungo FC yaichapa Fountain Gate FC mabao 2-1

MANYARA-Namungo FC kutoka Ruangwa mkoani Lindi imejikusanyia alama tatu kutoka kwa Fountain Gate FC ni kupitia ushindi wa mabao 2-1.
Mtanange huo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara umepigwa Desemba 25,2024 katika Dimba la CCM Kwaraa mjini Babati Mkoa wa Manyara.

Pius Buswita dakika ya 10 ndiye aliyefungua pazia la mabao kwa kulipa bili kwa waajiri wake Namungo FC maarufu kama wauaji wa Kusini.

Dakika ya 30', Salum Kihimbwa alisawazisha bao hilo ambalo lilidumu hadi kipindi cha mapumziko kwa pande zote ubao ukisoma bao moia moja.

Katika kipindi cha pili, Geoffrey Luzendaze aliwapatia waajiri wake bao dakika ya 78 ambalo lilidumu hadi dakika 90 za mchezo kufikia tamati.

Namungo FC chini ya Kocha Juma Mgunda imejikusanyia alama 17 baada ya mechi 16 na wanasalia nafasi ya 12 huku Fountain Gate FC wakisalia nafasi ya sita kwa alama 20 baada ya mechi 15 kwa sasa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news