Waliomteka mfanyabiashara Deogratius Tarimo wakamatwa

DAR-Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaaam limewakamata watu wanane wanaotuhumiwa kumteka mfanyabiashara Deogratius Tarimo katika eneo la Kiluvya, Ubungo Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro akiongea na waandishi wa gabari leo Desemba 4,2024 amesema,watuhumiwa hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti katika Mikoa ya Dar es salaam, Ruvuma na eneo la Mbingu, Mlimba Mkoani Morogoro.

“Pia lilipatikana gari aina ya Toyota Raum ambayo ilitumiwa wakati wa tukio hilo huku ikitumia namba isiyo halisi T 237 EGE na baada ya ufuatiliaji kufanyika imefahamika namba yake halisi ya gari hiyo ni T237 ECF,”ameeleza Kamanda Muliro.

Amewataja waliokamatwa kuwa ni Bato Bahati Tweve (umri Miaka 32 – Bondia), Yusuph Abdallah (32), Fredrick Juma (31), Nelson Elimusa Msela (24 - Dereva Tax), Benk Daniel Mwakalebela ‘Tall’ (40), Thomas Ephraim Mwakagile ‘Baba Mage’ (45), Anitha Alfred Temba (27) na Isack Mwaifani (Bondia).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news