NHC yaendelea kuhudumia wananchi katika Tamasha la Kimataifa la Maendeleo ya Filamu na Sanaa

DAR-Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa,Bi.Nyakaho Mahemba ametembelea banda la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Tamasha la Kimataifa la Maendeleo ya Filamu na Sanaa linaloendelea katika viwanja vya Posta jijini Dar es Salaam.
Tamasha hilo ambalo limeanza Desemba 11,2024 limeandaliwa na Bodi ya Filamu Tanzania ambapo linatarajiwa kufikia tamati Desemba 15,2024.
Katika tamasha hilo ambalo NHC wapo Banda Na. 18 wameshiriki kama wadau ili kuendelea kuwapa wananchi huduma mbalimbali wanazozitoa.

Aidha,Bi.Nyakaho Mahemba akiwa katika banda hilo amejifunza kuhusu huduma za shirika ikiwemo miradi mbalimbali inayotekelezwa na NHC kote nchini.

NHC ikiwa ni miongoni mwa taasisi za umma iliyopo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imekuwa na utaratibu wa kushiriki katika matukio mbalimbali ili kuhakikisha inawafikishia washiriki na wananchi elimu kuhusu huduma wanazotoa.
Miongoni mwa huduma wanazotoa ni pamoja na ujenzi wa nyumba za makazi, biashara ikiwemo ofisi kwa ajili ya kupangisha na kuuza katika maeneo mbalimbali nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news