NHIF:Uzinduzi wa mifumo na kifurushi cha Toto Afya Kadi (TAK) kufanyika Desemba 17,2024

DODOMA-Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama (Mb) anatarajia kuzindua Mfumo wa uandikishaji Wanachama, Mfumo wa Uchakataji Madai na Kifurushi cha Toto Afya Kadi Desemba 17,2024.
Uzinduzi wa Mifumo unafanyika baada ya Mfuko kutekeleza agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha Mifumo ya Serikali inasomana.

Aidha,kwa upande wa Toto Afya Kadi, Mfuko umefanya marejeo ya kifurushi hicho kwa kuzingatia mahitaji halisi ya kundi la watoto chini ya umri wa miaka 18, hali ya kipato cha wananchi pamoja na hali ya Mfuko.

Kutokana na hayo, mpango huo wa Toto Afya Kadi utazinduliwa rasmi kwa tarehe tajwa hapo juu.

Kwa sasa Mfuko unaendelea na utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote hususan katika usajili wa wanachama kupitia makundi mbalimbali ikiwemo kundi la Wanafunzi kuanzia ngazi ya Awali hadi Chuo Kikuu kwa gharama ya shilingi 50,400/=tu.

Mfuko unatoa rai kwa wananchi kuendelea kujiunga ili kuwa na uhakika wa huduma zamatibabu wakati wowote bila kikwazo cha fedha kupitia mtandao mpana wa vituo zaidiya 10,000 vya kutolea huduma nchi nzima.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news