Ofisi yetu itaendelea kuwa taasisi ya mfano-Mwanasheria Mkuu wa Serikali

DODOMA-Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari amewataka Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuendelea kusimamia misingi ya Weledi na Ubora katika utekelezaji wa majukumu yao.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameyasema hayo wakati wa kikao maalumu na Watumishi wa Ofisi Mwanasheria Mkuu wa Serikali kilichofanyika leo tarehe 03 Desemba, 2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho Mwanasheria Mkuu wa Serikali, amesema kikao hicho ni mahsusi kwa ajili ya kufahamiana na kuwakumbusha watumishi kuhusu kanuni na taratibu zinazopaswa kuzingatiwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya msingi ili kuifanya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuendelea kuwa mfano wa kuigwa katika taasisi za umma.
“Ilikuwa ni muhimu sana kuwa na kikao kama hiki ili tuweze kufahamiana vizuri na kuweza kuendelea kufanya kazi vizuri na kila mtumishi ajisikie vizuri kufanya kazi kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

"Nitaendeleza yote mazuri na kuleta mabadiliko chanya ambayo yataweza kutusaidia kama Taasisi kuweza kutimiza malengo yetu na malengo ya Taifa, pia kuifanya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali a place to be,” amesema Mhe. Johari.

Aidha, Mhe. Johari amesema kupitia kikao hicho ni matarajio yake kuwa Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wataboresha zaidi utendaji kazi wao kwa kutoa huduma iliyo bora, kwa wakati na kuzingatia maslahi ya Taifa.

Awali akimkaribisha Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Samwel Maneno amewasisitiza Watumishi wa Ofisi hiyo kufanya kazi kwa kuendelea kuzingatia na kufuata Dhima, Dira, Kauli Mbiu na Maadili ya msingi ya Ofisi na hivyo kuleta matokeo chanya katika utendaji kazi.
“Niwaombe watumishi wote wa Ofisi hii, tuendelee kuzingatia na kufuata Dira, Dhima na Maadili ya Msingi ili tuifikie Kauli Mbiu yetu ya Weledi na Ubora,"amesema Mhe. Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news