Polisi Arusha wataja barabara zitakazofungwa mkesha wa siku tatu wa mwaka mpya

ARUSHA-Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani wametaja barabara zitakazofungwa katika mkesha wa mwaka mpya ambao tayari umeanza huku likitaja njia mbadala zitazotumika kuepusha usumbufu.
Akitaja njia hizo Mkuu wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP Zauda Mohamed ametaja njia hizo kuwa ni kutoka mzunguko (roundabout) ya Jengo la Ngorongoro Tower kuelekea ofisi za Jiji la Arusha na kuelekea Mnara wa Saa.

SSP Zauda ameendelea kutaja barabara nyingine kuwa ni kuanzia makutano ya barabara ya Goliondoi na ya Joel Maeda maarfu Airtel kuelekea mzunguko wa barabara ya Mnara wa Saa maarufu Clock Tower.

Mkuu huyo wa usalama barabarani amesema barabara nyingine kuwa ni makutano ya barabara ya Goliondoi na barabara ya Uhuru zilipo Ofisi za Vodacom kuelekea mzunguko wa mnara wa saa.

Kadhalika ametaja barabara nyingine kuwa ni makutano ya barabara ya TANESCO na barabara ya Fire kuelekea mzunguko wa barabara ya mnara wa saa na barabara nyingine ni makutano ya barabara ya Kanisa na Barabara ya Nyerere hadi mzunguko wa mnara wa saa.

Aidha SSP Zauda ametoa wito kwa wananchi hususani watakaotumia barabara za katikati ya mji kutumia njia mbadala huku akiwahakikishia kuwa askari watakuepo barabarani kuwaelekeza barabara za kupita kuepusha foleni ambazo zitajitokeza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news