Polisi kata watakiwa kuendeleza ushirikiano na jamii

KILIMANJARO-Polisi Kata nchini wametakiwa kuendeleza ushirikiano mwema na jamii ili kusaidiana katika kuzuia uhalifu na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto nchini, Naibu Kamishna wa Polisi Maria Nzuki wakati akifunga mafunzo ya siku tano kwa Askari Kata kutoka Mikoa ya Dodoma, Tanga, Kinondoni na Temeke yaliyokuwa yakifanyika Shule ya Polisi Tanzania- Moshi mkoani Kilimanjaro.
DCP Nzuki amesema Jeshi la Polisi kwa sasa linaendelea kutekeleza mradi huo wa Polisi kata na umekuwa na mafanikiwa makubwa hivyo ushirikiano uliopo ni vyema ukaendelea ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Jamii kutoka Makao Makuu ya Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi Elisante Ulomi amesema mafunzo hayo yamewaongezea uelewa mpana hususani katika kuzuia makosa ya ukatili wa kijinsia huku mwakilishi wa Shirikia la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) ambao ndio wafadhili wa mafunzo hayo Bi Norah Loehr amesema Polisi kata hao wana kazi kubwa katika jamii katika kuzuia uhalifu.

Aidha,Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto, Kamishna Msaidizi wa Polisi Faidha Suleiman na Mkuu wa Shule ya Polisi Tanzania- Moshi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ramadhani Mungi nao wameelezea umuhimu wa mafunzo hayo kwa Polisi kata hao ambao wapo na jamii kwa karibu.
Katika mafunzo hayo ya siku tano mada mbalimbali zilitolewa na wataalamu mbalimbali wakiwemo Maofisa wa Polisi wastaafu kwa lengo la kuhakikisha kuwa Polisi Kata ambao wamesambazwa nchi nzima na Jeshi la Polisi ili kusogeza huduma kwa wananchi wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news